Utukufu (Misa Upendo)

Utukufu (Misa Upendo)
Performed by-
AlbumMISA UPENDO
CategoryTBA
ComposerJ. C. Shomaly
Views6,710

Utukufu (Misa Upendo) Lyrics

MISA UPENDO - UTUKUFU

  1. [s] Utukufu kwa Mungu juu
    [w] Utukufu na amani duniani
    Kwa watu wote wenye mapenzi
    Kwa watu wote wenye mapenzi
    mapenzi mema (utukufu) *2
  2. Tunakusifu tunakuheshimu,
    Twakuabudu tunakutukuza
    Tunakushukuru Mungu kwa ajili,
    Ya utukufu wako mkuu
    Ee Bwana Mungu, Mfalme wa Mbinguni,
    Mu-ngu Baba, Mungu mwenye enzi,
    Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee,
    Ee Bwana Mungu, ee Bwana Mungu
  3. Mwanakondoo mwana wake Baba,
    Uondoaye dhambi za dunia
    Utuhurumie utuhurumie,
    Pokea ombi letu ee Baba
    Mwenye kuketi kuume kwa Baba,
    tuhurumie utuhurumie
    Kwa kuwa kwa kuwa, ndiwe peke yako,
    mtakatifu mtakatifu
  4. Pekee Bwana mkuu Yesu Kristu,
    pamoja naye Roho Mtakatifu
    Katika katika utukufu wake,
    Mu-ngu Baba a-amina.