Misa Amecea
Misa Amecea |
---|
Performed by | - |
Album | Misa Amecea |
Category | Misa (Sung Mass) |
Composer | O. Kajwang |
Views | 44,533 |
Misa Amecea Lyrics
BWANA UTUHURUMIE (MISA AMECEA)
- [ s/a ] { Bwana utuhurumie (ee Bwana)
[ w ] Bwana utuhurumie } *2
- [ t/b ] { Kristu utuhurumie (ee Kristu)
Kristu utuhurumie } *2
- [ s/a ] { Bwana utuhurumie (ee Bwana)
Bwana utuhurumie } *2
UTUKUFU KWA MUNGU (AMECEA)
- [ t ] Utukufu kwa Mungu juu Mbinguni
[ w ] Na amani kote duniani
( Kwa watu ) wenye mapenzi mema
Tunakusifu Baba, tunakuheshimu,
Twakuabudu sisi tunakutukuza
- Twakushukuru Mungu kwa tukufu
Wako mkuu ewe Mungu mfalme
(Ee Baba) wa Mbingu Baba yetu
- Bwana wetu Mwokozi Yesu Kristu
Mwana wa pekee wake Mungu
(Uliye) Mwanakondoo wa Mungu
- Unayeziondoa dhambi zote
Za dunia utuhurumie
(Pokea) pokea ombi letu
- Wewe unayeketi kuume
Kwake Baba utuhurumie
(Sikia) sikia ombi letu
- Kwani pekee yako ndiwe Bwana
Peke yako mkuu na mkombozi
(Pekee) pekee Yesu Kristu
- Kwa umoja wa Roho Mtakatifu
Ndani yake Baba watukuzwa
(Ee Yesu) milele na milele
NASADIKI KWA MUNGU (MISA AMECEA)
- Nasadiki kwa Mungu mmoja - mimi nasadiki
Ndiye Baba yetu mwenyezi -
Mwumba mbingu pia dunia
Nasadiki kwa Yesu Kristu
- Mwana wa pekee wa Mungu -
Aliyezaliwa kwa Baba -
Akapata mwili kwa Roho -
Kazaliwa naye bikira -
- Kisha yeye kasulubiwa -
Kwa mamlaka yake Pilato -
Kwa ajili yetu kateswa -
Alikufa na akazikwa -
- Kafufuka katika wafu -
Akapaa juu Mbinguni -
Ameketi kuume kwake -
Mungu Baba yetu Mwenyezi -
- Ndipo atakapotokea -
Ili awahukumu wote -
Kwake Roho Mtakatifu -
Kwa kanisa la Katoliki -
- Ushirika wa watakatifu -
Ondoleo la dhambi zetu -
Nangojea ufufuko wa miili -
Na uzima wa milele -
MTAKATIFU ( MISA AMECEA)
- [ t ] Mtakatifu Mtakatifu Bwana - Mungu wa majeshi
[ s ] Mtakatifu Mtakatifu Bwana - Mungu wa majeshi
- Mbingu na dunia zimejaa zimejaa,
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako *2
Hosanna juu, hosanna juu *2 mbinguni
Mbarikiwa nayekuja
Mbarikiwa nayekuja mbarikiwa
Mbarikiwa nayekuja kwa jina, jina lake Bwana
FUMBO LA IMANI ( MISA AMECEA)
- Yesu Kristu alikufa, Yesu Kristu kafufuka
(Yesu) Kristu atakuja, atakuja kwetu tena
MWANAKONDOO WA MUNGU (MISA AMECEA)
- [ t ] Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi
Za dunia ee mwana utuhurumie
- [ s ] Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi
Za dunia ee mwana utuhurumie
- [ b ] Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi
Za dunia ee mwana utujalie amani