Utukufu (Misa Amecea)
Utukufu (Misa Amecea) |
---|
Performed by | - |
Album | Misa Amecea |
Category | TBA |
Views | 23,366 |
Utukufu (Misa Amecea) Lyrics
MISA AMECEA - UTUKUFU
- Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Na amani kote duniani
(Kwa watu) wenye mapenzi mema
|s/a| Tunakusifu Baba, tunakuheshimu,
Twakuabudu sisi tunakutukuza
|t/b| Kusifu tunakusifu, heshimu,
Twakuabudu abudu tunakutukuza
- Twakushukuru Mungu kwa ‘tukufu
Wako mkuu ewe Mungu mfalme
(Ee Baba) wa Mbingu Baba yetu
- Bwana wetu mwokozi Yesu Kristu
Mwana wa pekee wake Mungu
(Uliye) Mwanakondoo wa Mungu
- Unayeziondoa dhambi zote
Za dunia utuhurumie
(Pokea) pokea ombi letu
- Wewe unayeketi kuume
Kwake Baba utuhurumie
(Sikia) sikia ombi letu
- Kwani pekee yako ndiwe Bwana
Pekee yako mkuu na mkombozi
(Pekee) pekee Yesu Kristu
- Kwa umoja wa Roho mtakatifu
Ndani yake Baba watukuzwa
(Ee Yesu) milele na milele