Utukufu (Misa Amecea)

Utukufu (Misa Amecea)
ChoirTBA
AlbumMisa Amecea
CategoryTBA

Utukufu (Misa Amecea) Lyrics

MISA AMECEA - UTUKUFU

 1. Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
  Na amani kote duniani
  (Kwa watu) wenye mapenzi mema

  |s/a| Tunakusifu Baba, tunakuheshimu,
  Twakuabudu sisi tunakutukuza
  |t/b| Kusifu tunakusifu, heshimu,
  Twakuabudu abudu tunakutukuza
 2. Twakushukuru Mungu kwa ‘tukufu
  Wako mkuu ewe Mungu mfalme
  (Ee Baba) wa Mbingu Baba yetu
 3. Bwana wetu mwokozi Yesu Kristu
  Mwana wa pekee wake Mungu
  (Uliye) Mwanakondoo wa Mungu
 4. Unayeziondoa dhambi zote
  Za dunia utuhurumie
  (Pokea) pokea ombi letu
 5. Wewe unayeketi kuume
  Kwake Baba utuhurumie
  (Sikia) sikia ombi letu
 6. Kwani pekee yako ndiwe Bwana
  Pekee yako mkuu na mkombozi
  (Pekee) pekee Yesu Kristu
 7. Kwa umoja wa Roho mtakatifu
  Ndani yake Baba watukuzwa
  (Ee Yesu) milele na milele

Favorite Catholic Skiza Tunes