Login | Register

Sauti za Kuimba

Kivumbi Lyrics

KIVUMBI

@ D. Nkoko

 1. Hapo ndipo tulipomfurahia Bwana Mungu wetu
  Hirizi na mizimu yote viliposhindwa kusimama
  Shetani naye kivumbi kakitimua kakimbia

  {Hapo ndipo tukasema hebu Mungu aitwe Mungu
  Hapo ndipo tukasema yeye apewe sifa
  Hapo ndipo tukasema atawale Mungu milele } *2

 2. Tazama Bwana alipounyoosha mkono wake mkuu
  Wachawi wote wakakoma, mapepo na yakanyamaza
  Waganga na tunguri zao kwa aibu wakaduwaa
 3. Bwana alipoinua mkono hodari kwa wagonjwa
  Wakoma wakatakasika viziwi wakasikia
  Viwete wakarukaruka kwa furaha wamepona
 4. Jicho la Bwana lilipowaelekea watu waovu
  Hasira, chuki na majivuno vyote vikatoweka
  Kiburi na maringo yao hapo ndipo vikapotea
Kivumbi
COMPOSERD. Nkoko
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMNyumba ya Roho
CATEGORYTafakari
 • Comments