Nyumba ya Roho
Nyumba ya Roho | |
---|---|
Performed by | St. Kizito Makuburi |
Album | Nyumba ya Roho |
Category | Roho Mtakatifu (Pentecoste) |
Composer | Charles Ruta |
Views | 9,853 |
Nyumba ya Roho Lyrics
Mungu wangu nikujue mimi, Mungu wangu nikupende
Mungu nikutumikie, kisha niurithi ufalme Mbinguni * 2
(wewe) roho umenipa ee, (kisha) ukaihifadhi vizuri
(yaani) ndani ya mwili ee (kwani) mwili ni nyumba ya rho- Ndiwe mungu peke yako, wa kuabudiwa ni wewe
Nishike kitakatifu siku hiyo siku yako
nisilitaje kabisa bure jina lako Mwenyezi
Ulimi wa mwili wangu usiiponze roho yangu - Niwaheshimu wazazi, ili nisiwasononeshe
Uhai wa binadamu niuthamini yani nisiuue
Kuiba nijiepushe, kusema uwongo niache
Mwili wangu usizini ndipo roho yangu itapona - Niepuke kutamani yote yasiyo mali yangu
Naye mwanamke asiye mke wangu yani sio wangu
Hapo ndipo nitakuwa nimeutumia vizuri
Mwili ulioiumbia roho ifike Mbinguni juu