Bwana Ninakuita
Bwana Ninakuita | |
---|---|
Alt Title | Unifanye Niwe Chombo cha Amani |
Performed by | - |
Album | Iyelele |
Category | Injili na Miito (Gospel) |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 6,734 |
Bwana Ninakuita Lyrics
- Bwana ninakuita kwa maana utaitika
Utege sikio lako Mungu wangu
Bwana usikilize sala nayo maombi yangu
Unifanye niwe chombo cha amaniUnifanye niwe chombo cha amani ee Bwana
Unifanye mimi niwe nuru ya mataifa
Mashariki magharibi, niende
Niihubiri imani ya Bwana
Kaskazini na kusini niende
Niuhubiri upendo wa Bwana
{ Nitembee pande zote mimi Bwana, ee Bwana
Nikalitangaze neno lako kwa mataifa } *2 - Bwana uniongoze jina lako ni fimbo yangu
Wewe ndiwe ngao yangu niendapo
Bwana upendo wako nashindwa kusimulia
Na ninakupenda sana Mungu wangu - Bwana uniongoze niyashinde majaribu
Wewe ndiwe ngao yangu niendapo
Bwana watesi wangu tazama ni wengi sana
Niongoze nimshinde mwovu shetani