Uko Juu
Uko Juu |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 6,253 |
Uko Juu Lyrics
- Hufanani nasi, unang'ara na tena una enzi, una utukufu
Umepita zote, sifa tunazokutolea sisi, nao malaika oho
Wewe uko juu umetukuka na tunakuinua kwa nyimbo zetu hizi
- Walikuimbia, baba zetu lakini hazikwisha, sifa zako wewe
Na watakatifu, wanaimba na hazimaliziki, tenzi hazitoshi oho
- Mimea ya nchi, yaeleza inapopukutika, kuhifadhi maji
Kwamba wewe Bwana, hupungui unajua kuumba, hupitiwi neno oho
- Kinyonga mdogo, anageuka rangi kujilinda, bila ya bunduki.
Anafafanua, umakini ndani ya kazi yako, isiyo dosari oho
- Na uhimidiwe, wewe Baba yaani ndiwe Mwana, Roho Mtukufu,
Ulivyotukuzwa, enzi zile sasa hata milele, utukuzwe pote oho