Kipeperushe Kitambaa Chako
Kipeperushe Kitambaa Chako |
---|
Performed by | - |
Category | Ubatizo |
Views | 9,586 |
Kipeperushe Kitambaa Chako Lyrics
- [ t ] Jiangalie jinsi unavyoenenda,
ujiulize kama hivyo ni sawa
Ndugu rejea ahadi yako kumkataa Ibilisi muovu
[ t ] Dhamira yako inakuambia nini,
inakusuta au bado ni huru, sasa
Ndugu rejea ahadi yako kumfuata Bwana Yesu milele
Ewe Mwenzangu - kipeperushe kitambaa chako
Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
Kisichafuke - kipeperushe kitambaa chako
Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
Kiweke safi - kipeperushe kitambaa chako
Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
- Uliye naye kweli ni mzuri sana,
pia kumbuka yuko wako wa ndoa -
Uliyeapa ni wewe sio mwingine,
kushikamana naye yule mmoja, basi -
- Maendeleo kweli ni muhimu sana,
lakini na wenzako wanahitaji -
Hicho kipato ndicho ulichopimiwa,
au mwenzetu unachota zaidi, leo -
- Unatamani kuwa mwenye madaraka,
umejiandaaje kuyatumia -
Je ni halali watu tukakutukuza,
wakati yupo yule alokuumba, haya -
- Kumbuka Yesu alipigwa mijeredi,
kwa sababu ya haya unayotenda -
Akatundikwa mtini akiwa tupu,
kadhalilishwa mwisho akauawa, hivyo -
- Kumbuka kuwa siku ile inakuja,
matendo yako yote kuhesabiwa -
Ni heri leo ukitunze kitambaa,
siku ya mwisho kiwa bado cheupe, kweli -