Mimi Nimeumbika
   
    
     
         
          
            Mimi Nimeumbika Lyrics
 
             
            
- { Mimi oh! oh oh! mimi oh! oh oh!
 Niumbika mimi kweli napendeza } *2
 { Nitakuimbia, nitakuchezea
 Asante Baba kuniumba jinsi nilivyo } *2
- Nampenda Bwana kwa kuwa ananisikiliza
 Huisikiliza sauti yangu na dua zangu
 Hunitegea sikio lake nimwitapo yeye
 Kwa hivyo nitaliita jina lake siku zote
- Kamba za mauti ziliponizunguka mimi
 Shida za kuzimu zikaniandama sana
 Niliona tabu nyingi nikamlilia Bwana wangu
 Nami nikaliita jina lake akaniokoa
- Bwana katujalia sauti nzuri ya kupendeza
 Ili tumwimbie yeye siku zote maishani
 Kwa hivyo yatupasa sote kumwimbia yeye
 Kwani Mungu wetu ni mkarimu kwa watu wote