Mimi Nimeumbika Lyrics

MIMI NIMEUMBIKA

@ Emmanuel Kawa

{ Mimi oh! oh oh! mimi oh! oh oh!
Niumbika mimi kweli napendeza } *2
{ Nitakuimbia, nitakuchezea
Asante Baba kuniumba jinsi nilivyo } *2

 1. Nampenda Bwana kwa kuwa ananisikiliza
  Huisikiliza sauti yangu na dua zangu
  Hunitegea sikio lake nimwitapo yeye
  Kwa hivyo nitaliita jina lake siku zote
 2. Kamba za mauti ziliponizunguka mimi
  Shida za kuzimu zikaniandama sana
  Niliona tabu nyingi nikamlilia Bwana wangu
  Nami nikaliita jina lake akaniokoa
 3. Bwana katujalia sauti nzuri ya kupendeza
  Ili tumwimbie yeye siku zote maishani
  Kwa hivyo yatupasa sote kumwimbia yeye
  Kwani Mungu wetu ni mkarimu kwa watu wote
Mimi Nimeumbika
COMPOSEREmmanuel Kawa
CHOIRSt. Don Bosco Kyaani
ALBUMWashuhuda wa Yesu
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments