Nyanyukeni Waumini
   
    
     
         
          
            Nyanyukeni Waumini Lyrics
 
             
            
- { Nyanyukeni waumini wote tufanye shangwe
 Kwa nderemo, kwa vigelegele na kwa vifijo } *2
 Bwana asifiwe (sana) Bwana asifiwe (kweli)
 Bwana asifiwe Mwathani aragoshuo
- Nikiziangalia mbingu ni kazi ya vidole vyake
 Mwezi na nyota za mbinguni ulizoratibisha wewe
- Uwezo wake Bwana Mungu haupimiki kwa mizani
 Mipango yake kwetu sisi haiwezi kubadilishwa
- Alikausha baharà ya Shamu ikawa nchi kavu
 Waisraeli wakapita kwa uwezo wa Mungu Baba
- Na tupigeni tarumbeta vinubi hata na matari
 Tuimbe wimbo wake Musa na ule wa Mwanakondoo
- Pazeni sauti zenu kwa shangwe hata na vifijo
 Sifa pia na utukufu tumpe Bwana siku zote