Rafiki Yangu Njoo
   
    
     
         
          
            Rafiki Yangu Njoo Lyrics
 
             
            
- Rafiki yangu njoo kaa chini, nisikilize kwa makini
 Rafiki njoo kaa chini ,nikueleze jambo moja aah
 
 {Kila mtu atalipwa sawasawa na matendo ooh
 Kila mtu atalipwa sawa nayo matendo yake } * 2
 
- Kama uliua kwa upanga, utakufa kwa upanga
 Uliua kwa silaha, utakufa kwa silaha aah
- Kama ulikuwa ni mzinzi, utakufa kwa uzinzi
 Ulikuwa mzinifu, utakufa kwa uzinzi iih
- Kama ulikuwa mfitini, utalipwa ufitini
 Ulikuwa mfitini, utalipwa ufitini iih
- Kama ulikuwa mkarimu, utalipwa ukarimu
 Ulikuwa ni mchoyo, utalipwa sawa na choyo ooh
- Kama ulinitendea wema, utalipwa matendo mema
 Ulinitendea baya, utalipwa kwa ubaya aah