Sadaka ya Uchungu
| Sadaka ya Uchungu |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Faith |
| Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
| Views | 7,349 |
Sadaka ya Uchungu Lyrics
{ Sadaka ya uchungu na kitubio cha machozi
Vitanifaa nini kama nisipolainisha moyo } *2
- Moyo wangu mgumu tena mgumu kama jiwe
Na kumwagia maji juu ya jiwe kazi bure
- Nisipolitangaza pendo la Mungu kwa vitendo
Kamwe sitazionja baraka na rehema zake
- Na nisipoikiri kanuni ile ya imani
Hata nikeshe mimi kwa maombi ni kazi bure
- Ni heri nikubali kikao cha upatanishi
Nimkane shetani na nguzo zake nizivunje