Uje Roho Mtakatifu, Uje Mfariji

Uje Roho Mtakatifu, Uje Mfariji
Performed bySauti Tamu Melodies
CategoryRoho Mtakatifu (Pentecoste)
Composer(traditional)
VideoWatch on YouTube
Views43,782

Uje Roho Mtakatifu, Uje Mfariji Lyrics

  1. Uje Roho Mtakatifu, uje mfariji

  2. Uje baba wa masikini - uje mfariji
    Roho mtoa vipaji - uje mfariji
  3. U rafiki mwema sana -
    U mfutaji wa machozi -
  4. Uwe mwanga wa mioyo -
    Tuangaze toka mbinguni -
  5. Tia nuru akilini -
    Na mapendo mioyoni -
  6. Osha machafuko yetu -
    Na kuponya majeraha -
  7. Uregeze ukaidi -
    Pasha moto ubaridi -
  8. Bila nguvu yako wewe -
    Mwanadamu hana kitu -
  9. Kwenye kazi u pumziko -
    Kwenye joto burudisho -
  10. Ufukuze mashetani -
    Na amani tupe hima -
  11. Wape waamini wako -
    Paji zako zote saba -