Wangu wa Milele

Wangu wa Milele
Performed by-
CategoryHarusi
ComposerS. Ndibalema
Views6,944

Wangu wa Milele Lyrics

 1. Mpenzi wangu ungana nami, tumshukuru Mungu wetu
  Uje tucheze kwa furaha, tumshukuru Mungu wetu
  Kwani ile siku tuliyoingojea - iwe tumshukuru Mungu wetu
  Mwenyezi ametujalia - iwe, tumshukuru Mungu wetu

 2. Nasema mbele ya wazazi wako (ni wewe)
  Ni wewe niliyekuchagua (ni wewe)
  Nasema mbele ya wazazi wangu, ni we wangu wa moyoni
  Ninatamka mbele za Mungu (ni wewe)
  Mtima wangu nakupatia (ni wewe)
  Nasema mbele ya wazazi wangu, Ni we wo mtima gwange
 3. Unawaacha wazazi wako (ni wewe)
  Mwili mmoja tunakuwa (ni wewe)
  Nami nitakupenda milele, Ni we wangu wa moyoni
  Ninawaacha wazazi wangu (ni wewe)
  Mwili mmoja tunakuwa (ni wewe)
  Nami nitakupenda milele, Ni we wo mtima gwange
 4. Ndi-we mama wa watoto wangu (ni wewe)
  Mwenyezi Mungu kanipatia (ni wewe)
  Karibu kwetu kipenzi changu, ni we wangu wa moyoni
  Ndi-we baba wa watoto wangu (ni wewe)
  Mwenyezi Mungu kanipatia (ni wewe)
  Nakuja kwenu kipenzi changu, Ni we wo mtima gwange
 5. Nawashukuru wazazi wako, umbo zuri wameniletea
  Namshukuru Mwenyezi Mungu, ni we wangu wa moyoni
  Nawashukuru wazazi wako, lulu yangu walinitunzia
  Haki ya Mungu nitakutunza, ni we wo mtima gwange
Kihaya Melody