Kikondoo cha Mungu

Kikondoo cha Mungu
Performed by-
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJohn Mgandu
Views9,387

Kikondoo cha Mungu Lyrics

  1. { Kikondoo cha Mungu, mkate wa Mbinguni
    Mlishi wa roho zetu, nakuabudu }*2

  2. U Babangu mwema, na msimamizi
    Mpaji wa uzima, wangu mwokozi
  3. Fumbo abudiwa, nakuamini
    Kaza Yesu mpendwa, yangu imani
  4. Mlo wa roho yangu, hostia nzima
    Niwie ya mbingu, kweli amana
  5. Ee Rabbi mtu Mungu, unirizishe
    Njoo shuka kwangu, kanishibishe
  6. Anakaribia, mpenzi amini
    Ataka ingia mwangu moyoni