Jenga Urafiki na Yesu

Jenga Urafiki na Yesu
Performed bySt. Maurus Kurasini
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerSindani P. T. K
Views18,584

Jenga Urafiki na Yesu Lyrics

  1. { Jenga urafiki na Mwokozi Yesu,
    amana ya Mbingu kurithishwa } * 2
    { Tembea na yeye upendavyo,
    safiri na yeye uwezavyo
    Kula na yeye popote pale } * 2

  2. Anza basi leo kuwa na yeye,
    Rafiki wa kweli katika Mbingu, usichelewe kuwa na yeye
  3. Ni kinga kamili ukiwa naye,
    Kwa taabu zako popote pale, anayajua maisha yako
  4. Kwa magonjwa yako ndiye tabibu,
    Ayajua yote magonjwa yako, ongozana naye utapona
  5. Jibu la maisha ukiwa naye,
    Anapokuwapo hana mpinzani, jipendekeze unufaike
Recorded by * St. Maurus Kurasini Arusha * St. Cecilia Tabora