Furaha Hiyo Niliyo Nayo
Furaha Hiyo Niliyo Nayo | |
---|---|
Performed by | St. Michael Otiende Lang'ata |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | M. Z. Yohana |
Views | 4,185 |
Furaha Hiyo Niliyo Nayo Lyrics
Furaha hiyo niliyo nayo yatoka kwa Mungu *2
{Ndiye Baba (baba), ninayemtumaini (baba)
Kwenye maisha yangu, Yeye ndiye kimbilio} *2 Baba- Sina budi kumshangilia Mungu
Baba kwa huruma yake na wema wake
Mema mengi aliyonitend`a mimi
Sina budi kushukuru asante Baba - Yeye ndiye tumaini langu mimi
Ndiye msaada wangu na wokovu wangu
Bila Mungu mimi siwezi chochote
Sina ujanja wowote ni ubatili - Ni wangapi, walimpuuza Mungu
Kwa kukiuka sheria wakapata fimbo
Wakarudi, wakamlilia Mungu,
Kuomba huruma yake, akawasamehe - Nawe ndugu kujiona we mdhambi
Mungu anakutafuta urudi kwake
Nenda hima ukatubu dhambi zako,
Ukaipate furaha iliyo ya kweli