Imeandikwa Wapi
   
    
     
        | Imeandikwa Wapi | 
|---|
| Alt Title | Nimefungua Vitabu Vyote | 
| Performed by | St. Cecilia Mavurunza | 
| Album | Nimefungua Vitabu Vyote | 
| Category | Tafakari | 
| Composer | Victor Aloyce Murishiwa | 
| Views | 5,806 | 
Imeandikwa Wapi Lyrics
 
             
            
- Nimefungua vitabu vyote nikapekua kurasa zote
 Kulitafuta andiko hili sikuliona
 Ni wapi palipohalalishwa matendo haya
 machafu sana yachafuayo jamii yetu sikupaona
 Fungua macho mkristu, fungua macho
 Giza nene limetanda, fungua macho
 Ni wakati wa kukesha, fungua macho
 Shetani katuzunguka, fungua macho
 Imeandikwa wapi kwamba ushoga ni halali?
 Wapi palipoandikwa rushwa ni funguo ya haki?
 (tena) Imeandikwa wapi kwamba hirizi ni halali?
 Wapi imehalalishwa wanaume kufunga ndoa?
 (hiyo) Imeandikwa wapi, imeandikwa wapi?
 Kurasa zote hakuna!
 Imeandikwa wapi imeandikwa wapi?
 Sheria zake Mungu!
- Kemea Mkristu matendo hayo
 Kwa sakramenti zote uyasafishe
 Epukana nayo matendo hayo
 Kwa sakramenti zake uyasafishe
- Ingia katika shamba la Bwana
 Mambo ya ulimwengu ni machafuko
 Tembea katika shamba la Bwana
 Zitende kazi zake kwa moyo safi
- Njia zake Bwana usiziache
 Ni barabara safi zenye amani.
 Sheria za Bwana usiziache
 Na maagizo yake ni ya Adili