Hiki Kiza

Hiki Kiza
ChoirSt. Cecilia Zimmerman
CategoryTafakari

Hiki Kiza Lyrics

 1. Hiki kiza ni kiza kinene kimetanda ulimwenguni
  Kimeyatikisa mataifa makabila mbalimbali
  Familia hata majirani makabila hawaelewani
  Ofisini hata makazini amani hakuna tena

  Twalia twaomba amani (amani amani)
  Twaomba amani twaomba amani, amani, amani
  Watu wengi sasa wameangamia
  Wazee watoto nao wateseka
  Amani haipo tena duniani Bwana twaomba amani

 2. Pande nyingi watu wamekufa sababu yake ni mizozano
  Majirani hawaelewani sababu ya ukabila
  Imekuwa sasa kawaida watoto kuwadharau wazazi
  Kusema eti wazazi wao wamepitwa na wakati
 3. Migogoro watu mbali mbali taifa na taifa lingine
  Wanadamu sasa ni wakali hata kuliko wanyama
  Msamaha tumeusahau amri za Mungu tumeziacha
  Kila mtu ajiona yeye sasa tutakwenda wapi
 4. Sikieni taifa la Mungu ujumbe huu twawapatia
  Mambo haya tunayoyafanya siku moja tutalipa
  Mwisho wetu utakapofika utajibu nini kwa Mungu
  Atakapotuhukumu sisi kila mtu kadiri yake