Ee Nafsi Yangu
| Ee Nafsi Yangu | |
|---|---|
| Performed by | St. Maurus Kurasini |
| Album | Hubirini Kwa Kuimba |
| Category | Zaburi |
| Views | 6,759 |
Ee Nafsi Yangu Lyrics
{ Ee nafsi yangu mhimidi Bwana, wewe Bwana Mungu wangu,
umejifanya mkuu sana, umejivika heshima na adhama } * 2- Umejivika nuru kama vazi, umezitandaza mbingu kama pazia
Na kuziweka nguzo za horofa, nguzo za horofa zake majini - Huwafanya malaika zake, huwafanya kuwa pepo
Na watumishi watumishi wake, huwafanya kuwa moto wa miali - Ee Bwana jinsi yalivyo mengi, yalivyo mengi matendo yako
Kwa heshima umefanya vyote, dunia imejaa mali yako