Kristu Pasaka Wetu (Sekwensia)

Kristu Pasaka Wetu (Sekwensia)
Performed by-
CategoryTBA
Views12,690

Kristu Pasaka Wetu (Sekwensia) Lyrics

  1. Kristu Paska yetu, amechinjwa sadaka;
    tuile karamuye, na twimbe Aleluya
  2. Aliyejitoa, sadaka ya Paska,
    wakristu wamtolee, sadaka ya Sifa.
  3. Mwanakondoo aliwakomboa kondoo, Kristu asiye na dhambi
    amewapatanisha na Baba, watu wenye dhambi.
  4. Mauti na uzima, vimeshindana ajabu;
    Mkuu wa uzima aliyekufa, atawala mzima.
  5. Utuambie Maria, uliona nini njiani?
    Niliona kaburi la Kristu Mzima,
    na Utukufu wa aliyefufuka.
  6. Mashahidi ni Malaika,
    Leso ya uso na mavazi
    Kristu tumaini langu kafufuka,
    awatangulia Galilaya.
  7. Twajua Kristu amefufuka, kweli katika wafu
    Ewe Mfalme mshindaji, Utuhurumie.
  8. Amina Aleluya, Amina Aleluya *2