Bwana u Sehemu Yangu
Bwana u Sehemu Yangu | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Views | 102,082 |
Bwana u Sehemu Yangu Lyrics
- Bwana u sehemu yangu, rafiki yangu wewe
Katika safari yangu, tatembea na wewe
Pamoja na wewe, pamoja na Wewe
Katika safari yangu, tatembea na wewe. - Mali hapa sikutaka, ili niheshimiwe,
Na yanikute mashaka, sawasawa na wewe
Pamoja na wewe, pamoja na wewe
Heri nikute mashaka sawasawa na wewe. - Niongoze safarini Mbele unichukue
Mlangoni mwa Mbinguni, niingie na wewe
Pamoja na wewe, pamoja na wewe
Mlangoni mwa Mbinguni, niingie na wewe