Tunakushukuru Mama Maria
Tunakushukuru Mama Maria | |
---|---|
Choir | St. Cecilia Mwenge Dsm |
Album | Tunakushukuru Mama Maria |
Category | Bikira Maria |
Composer | P. F. Mwarabu |
Source | Tanzania |
Tunakushukuru Mama Maria Lyrics
Tunakushukuru Mama Maria,
Kwa neema unazotujalia
Asante mama wa Yesu uliye na huruma
Uzidi kutuombea mpaka saa ya kufa
-
Mama wa Yesu, mama mfariji wetu
Asante sana kwa kutusimamia -
Neema zako zinatututia nguvu
Asante mama Maria mtakatifu -
Tuna furaha, tuna matumaini
Kwa kuwa tunawe mama wa huruma -
Mama wa Yesu, wee Mama Maria
Tusaidie tushinde vishawishi -
Katika mbingu ndiwe mbarikiwa
Katika maisha ndiwe kinga yetu