Nitajisifia Udhaifu Wangu
Nitajisifia Udhaifu Wangu |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Composer | Marcus Mtinga |
Views | 3,558 |
Nitajisifia Udhaifu Wangu Lyrics
Nitajisifia udhaifu wangu udhaifu wangu,
ili uweza wa Kristu ukae juu yangu
maana ninapokuwa dhaifu ndipo nilipo na nguvu x2
- Sina budi kujisifia japo kuwa haipendezi,
lakini ninajizuia nisihesabiwe hatia,
bali nasema ukweli juu ya maono niliyopata.
- Sababu ya mafunuo hayo nalipewa mwiba mwilini,
nikamsihi Mungu wangu jambo hili liniepuke,
naye akaniambia neema yangu pekee inatosha.
- Napendezwa na udhaifu dharau taabu mateso,
nakuyavumilia yote hayo kwa ajili ya Kristu,
kwani uweza wa Kristu hutimia katika udhaifu.