Asante Mungu
Asante Mungu | |
---|---|
Performed by | St. Joseph the Worker Ngokolo Shinyanga |
Album | Njooni Tumsifu Mungu |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 24,854 |
Asante Mungu Lyrics
- Ehee nakumbuka kule nilikotoka;
Ahaa najiuliza mimi nisemeje
Ehee kigugumizi kinanikamata;
Ahaa najiuliza mimi najihoji tuSina neno mimi sina jipya la kusema,
umetenda wema mpaka unanishangaza.
Nashukuru Bwana asante Mungu tena sana asante,
asante Mungu sina maneno asante asante Mungu - Ehee ulinigusa tumboni mwa mama ...
Ehee nikazaliwa tayari kwa kazi ... - Ehee ukanipa kuwainua watu ...
Ehee wakakuimbia na kukusifu ... - Ehee dunia iliponishambulia ...
Ehee ukasimama ukanitetea ... - Ehee nitakuimbia na nyumba yangu ...
Ehee tutakusifu siku za uhai ...
Hitimisho
Ama kweli iya unanishangaza wewe ni mwema,
Ama kweli iya unapenda watu wewe ni mwema,
Ama kweli iya unawathamini wewe ni mwema,
Nashukuru hiya Nashukuru sana wewe ni mwema
Nakusifu hiya nakusifu sana wewe ni mwema
Siku zote hiya nitakuimbia wewe ni mwema
we ni mwema wewe ni mwema (ni mwema)
wewe ni mwema na mpole wewe ni mwema
ni mwema wewe ni mwema ni mwema Hiya
Recorded by
* Kwaya ya Mtakatifu Yusufu Mfanyikazi, Ngokolo Shinyanga
* St. Monica Kigamboni