Dira
Dira | |
---|---|
Alt Title | Asipojenga Nyumba |
Performed by | Kwaya ya Malkia wa Mitume Parokia ya Vincent Palloti Arusha |
Album | Dira |
Category | Tafakari |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 5,338 |
Dira Lyrics
Asipojenga nyumba wale waijengao
wanafanya kazi bure na wanapoteza muda
Na wanaoulinda mji wanapoteza usingizi
maana wanakesha bure wao si lolote si kitu
Hakuna jema nje ya Mungu, hakuna mali pasipo yeye
Hakuna ushindi bila Mungu wala kufanikiwa asipokuwapo
{(Yeye) Ni nguzo ya yote, nguzo ya kila kitu
Ni uwezo wote na sababu ya mema yote
(Yeye) ni dira (aoh) daima tumtangulize * 2 } *2- Ewe tajiri mali uliyo nayo isalimishe
mikononi mwake Mungu - Nawe msomi vyeti ulivyo navyo ni vumbi tupi
kama hujampa Mungu - Ewe mzima, nguvu na afya na uhai ni bure
Kama havilindi Mungu - Kuumwa kwako na shida zako zitakuangamiza,
kama hujampa Mungu
Ni nguzo yetu na dira yetu
Ni ngao yetu milele