Msamaha ni Maua
| Msamaha ni Maua | |
|---|---|
| Alt Title | Narudi zangu Mimi | 
| Performed by | BMT Ledochowska K/Ndege Dodoma | 
| Album | Kimbunga | 
| Category | Tafakari | 
| Composer | Bernard Mukasa | 
| Views | 9,625 | 
Msamaha ni Maua Lyrics
- Narudi zangu mimi kwa upatanisho
 Narudi kwa amani turudiane (aiyo)
 Niliyokukosea unisamehe
 Na uliyonikosea nimekusamehe ndugu yangu
 Narudi zangu mimi kwa upatanisho (ninatafuta amani)
 Narudi kwa amani turudiane (yelele)
 Niliyokukosea unisamehe (na)
 Uliyonikosea nimekusamehe ndugu yangu
- Ubinadamu wetu ulituangusha
 tukajeruhiana mioyo yetu (aiyeiye)
 Lakini leo wangu, tufarijiane,
 tuyaache ya nyuma sasa tuanze upya kabisa
- Tulipokwaruzana, tulijichafua,
 Tukampa jeuri yule muovu (aiyeiye)
 Tukipatana leo ataaibika
 Haya tumuaibishe sasa tuanze upya kabisa
- Nipe mkono wako tukumbatiane
 Jamii ijifunze kutoka kwetu (aiyeiye)
 Sogeza shavu Basi na tunusiane;
 Busu lenye amani (sasa) tuanze upya kabisa.
 Kusameheana kunamleta Yesu katikati ya watu
 Kusamehe ni maua
 Kunapumzisha kunalegeza mwili kunafungua roho
 kusamehe ni maua
 Inapendeza sana msamaha ni maua
 Inavutia sana msamha ni maua
 Inapamba nafsi msamaha ni maua
 Inafungua mbingu msamaha ni maua
Recorded by several Tanzanian choirs including
* Kwaya ya Mwenye Maria Theresa, Ledowchoska, Parokia ya Uwanja wa Ndege Dodoma Tanzania
* Kwaya ya Mt. Francisco Kwa Ngulelo Arusha
and others
  
 
 
 
  
         
                            