Yowe la Mwisho

Yowe la Mwisho
ChoirTBA
AlbumYowe la Mwisho
CategoryTBA
ComposerBernard Mukasa
Musical Notes
Time Signature6/8
Music KeyKey E

Yowe la Mwisho Lyrics

YOWE LA MWISHO

 1. Ee Mungu ukifuatilie kilio chetu
  Nazo sala kwa ajili ya usalama wetu


  Ni wewe uliye tegemeo utulinde daima milele
  Kwako tumejikabidhi, utulinde daima milele
  Ulivyowavusha Wayahudi, utulinde daima milele
  Baharini kwa miguu, utulinde daima milele
  Ukumbuke ahadi yako, utulinde daima milele
  Aombaye utampa, utulinde daima milele
 2. Tumekuita na kwa sauti na kwa machozi mengi
  Uko kimya lakini twajua utaitika
 3. Wanaotupenda wameungana kutuombea
  Usiache magoti yao yachubuke bure
 4. Malaika na watakatifu wanatuombea
  Wasikie kwa sababu umependezwa nao
 5. Yakumbuke maumivu ya Yesu msalabani
  Ukubali yawe badala ya mateso yetu


  Tunakwama sauti makoo yamechoka
  Fanya hima mwenyezi uje utuokoe
  Hayatoki machozi ona yamekauka
  Tutalia na nini wahi utuokoe
  Ewe Rabi Mungu yowe la Mwisho tunapiga utusikie * 2
  Ewe Rabi Mungu yowe la Mwisho tunapiga uwiii
  Yowe la Mwisho tunapiga utusikie