Utanisahau Kabisa Mpaka Lini
Utanisahau Kabisa Mpaka Lini | |
---|---|
Alt Title | Ee Mwenyezi Mungu |
Performed by | Maria Mt Mama wa Mungu Musoma |
Album | Matumaini ya Safari |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | Marcus Mtinga |
Views | 5,436 |
Utanisahau Kabisa Mpaka Lini Lyrics
- Ee Mwenyezi Mungu utanisahau kabisa mpaka lini?
Utauficha uso wako mbali nami mpaka lini Mungu wangu? - Roho na mwili wangu vitakuwa na wasiwasi mpaka lini?
Na masikitiko siku hata siku sina raha maishani - Bwana nimelia sana, mchana uko wapi unifadhili
Na usiku usingizi sipati nakesha nikiwaza - Nimedhoofika sana fimbo kila siku nachapwa nimekonda
Sina pa kukimbilia njia zote zimelindwa niende wapi - Maadui zangu ni wengi, njaa magonjwa ya hatari na ajali
Vita vimepamba moto dunia yote ona Bwana ninavyotishwa - Ndugu na rafiki zangu wametoweka siwaoni wako wapi
Kama wako kwako Bwana nambie nami nijaribu kuwafuata - Yesu wangu u Mungu wangu njoo haraka nakuita njoo Bwana
Mwanao nateseka sijiwezi mimi ninaomba msaada wako - Ninainua mikono taabu mateso maumivu yangu yote
Ninakukabidhi wana yapokee Mwokozi naomba usinitype