Yesu Njoo Rohoni Mwangu
Yesu Njoo Rohoni Mwangu | |
---|---|
Performed by | Maria Mt Mama wa Mungu Musoma |
Album | Matumaini ya Safari |
Category | Ekaristia (Eucharist) |
Composer | D. Kizange |
Views | 10,239 |
Yesu Njoo Rohoni Mwangu Lyrics
Yesu njoo rohoni mwangu, karibu nakukaribisha
Naumia rohoni mwangu, njaa kiu vinanitesa
{ Kimbilio langu ni wewe, nimekuja unilishe
Mwili wako na damu yako, nipate uzima milele } *2
Yesu njoo rohoni mwangu, nipate faraja milele- Najongea meza yako, japo sifai kabisa
Wewe wanikaribisha na uovu wangu wote - Yesu wangu nguvu yangu, unilishe mwili wako
Wewe ndiwe tegemeo la maisha yangu yote - Wewe ndiwe kitulizo cha Roho yangu milele
Bila wewe sina nguvu roho yangu ni dhaifu - Mwili wako ni chakula damu yako ni kinywaji
Unilishe uninyweshe siku zote kaa name