Yesu Njoo Rohoni Mwangu

Yesu Njoo Rohoni Mwangu
ChoirMaria Mt Mama wa Mungu Musoma
AlbumMatumaini ya Safari
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerD. Kizange
Musical Notes
Time Signature2
4
Music KeyB Flat Major

Yesu Njoo Rohoni Mwangu Lyrics

Yesu njoo rohoni mwangu, karibu nakukaribisha
Naumia rohoni mwangu, njaa kiu vinanitesa
{ Kimbilio langu ni wewe, nimekuja unilishe
Mwili wako na damu yako, nipate uzima milele } *2
Yesu njoo rohoni mwangu, nipate faraja milele

 1. Najongea meza yako, japo sifai kabisa
  Wewe wanikaribisha na uovu wangu wote
 2. Yesu wangu nguvu yangu, unilishe mwili wako
  Wewe ndiwe tegemeo la maisha yangu yote
 3. Wewe ndiwe kitulizo cha Roho yangu milele
  Bila wewe sina nguvu roho yangu ni dhaifu
 4. Mwili wako ni chakula damu yako ni kinywaji
  Unilishe uninyweshe siku zote kaa name