Ee Bwana Unikumbuke
Ee Bwana Unikumbuke | |
---|---|
Alt Title | Ee Mwana wa Mungu |
Performed by | Maria Mt Mama wa Mungu Musoma |
Album | Matumaini ya Safari |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | John Mgandu |
Views | 7,435 |
Ee Bwana Unikumbuke Lyrics
(Ee Mwana wa Mungu unifanye leo nishiriki
kwenye karamu yako karamu ya kiroho )* 2
(Sitaifunua siri kwa adui zako
Wala mimi sitakupa busu kama lile la Yuda) * 2
Bali kama yule mwizi
Ninakuomba ee Bwana unikumbuke mimi katika ufalme wako- Ninakuabudu Bwana kifulifuli,
Enzini uliyefichika Mungu uliye hai
Ulipo kweli chini ya maumbo haya,
Ya mkate pia divai ninajinyenyekeza
Karibu kwangu Bwana njoo ukae nami - Huu ni mwili na damu kweli ni hakika
Nikiona nigusa tena nikionja
Ni Yesu mwenyewe mimi pia ninasadiki
Aliyejitoa kwa ajili ya ulimwengu
Fumbo hili ni la kweli imani inaelewa - Kila ninapopokea komunyo takatifu
Ninarudishiwa nguvu mpya bila shaka
Ekaristi huimarisha mapendo moyoni
Yadumisha amani furaha iliyopotea
Hii hakika ni dawa safi ya roho