Ee Bwana Unikumbuke

Ee Bwana Unikumbuke
Alt TitleEe Mwana wa Mungu
ChoirMaria Mt Mama wa Mungu Musoma
AlbumMatumaini ya Safari
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerJohn Mgandu

Ee Bwana Unikumbuke Lyrics

(Ee Mwana wa Mungu unifanye leo nishiriki
kwenye karamu yako karamu ya kiroho )* 2
(Sitaifunua siri kwa adui zako
Wala mimi sitakupa busu kama lile la Yuda) * 2
Bali kama yule mwizi
Ninakuomba ee Bwana unikumbuke mimi katika ufalme wako

 1. Ninakuabudu Bwana kifulifuli,
  Enzini uliyefichika Mungu uliye hai
  Ulipo kweli chini ya maumbo haya,
  Ya mkate pia divai ninajinyenyekeza
  Karibu kwangu Bwana njoo ukae nami
 2. Huu ni mwili na damu kweli ni hakika
  Nikiona nigusa tena nikionja
  Ni Yesu mwenyewe mimi pia ninasadiki
  Aliyejitoa kwa ajili ya ulimwengu
  Fumbo hili ni la kweli imani inaelewa
 3. Kila ninapopokea komunyo takatifu
  Ninarudishiwa nguvu mpya bila shaka
  Ekaristi huimarisha mapendo moyoni
  Yadumisha amani furaha iliyopotea
  Hii hakika ni dawa safi ya roho