Ee Yesu Unihurumie
Ee Yesu Unihurumie | |
---|---|
Alt Title | NInakuungamia Mungu Wangu |
Performed by | - |
Album | Matumaini ya Safari |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | Marcus Mtinga |
Views | 8,559 |
Ee Yesu Unihurumie Lyrics
- Ninakuungamia Mungu wangu mpendwa wangu,
Tazama najilaza miguuni kwa majuto
Ee Bwana ninakuomba unitazame kwa huruma
Nalia nahuzunika kwa kuwa mimi nimwenye dhambi
Ni mambo ya ovyo ovyo na upuuzi zinaniponza
Kupenda mambo ya giza, hasira wivu, kiburi choyo - Ee Bwana ninakiri udhaifu wangu wo-te,
Unaujua wazi sidiriki kudanga-nya,
Na sasa naona haya kwa dhambi nyingi nilizo nazo,
nachoka kuishi ji-nsi nilivyo ninaona uchungu.
Unihurumie, unisamehe Bwana ninaumia,
ninasikitika ho-fu ni kubwa mwili hauna nguvu. - Popote nipitapo watu hunisema sa-na,
Ni wengi hunifyonya hutikisa vichwa vya-o,
Ni maisha gani haya tazama Bwana yanavyotisha,
sina mbele wala nyu-ma mi-mi kweli ninashangaza.
Tamaa za mwili ona zinavyoiangamiza roho,
adhabu inayoku-ja hakika ni ngumu kuitaja. - Ee Yesu ulikufa kwa ajili yangu mi-mi,
Lakini ona sasa nilivyochanganyiki-wa,
Si m--tu si mnyama ninasi-kitisha sana,
wanyama ndege sama-ki wadudu nao wanashangaa.
Wanataka kunitenga sijui sasa niende wapi,
Ee Yesu nihurumi-e nisaidie mwokozi wangu. - Ee Yesu ndiwe nguvu kwa wanyonge na dhai-fu,
Naomba unigeuze niwe mtu mnyo-fu,
Niuvue mwili mwovu na kwa hasira utupwe mbali,
ni maisha gani ha-ya taabu nyingi huzuni tele.
Niwavute watu wengi wakufuate mwokozi wangu,
na mwisho nifike kwa-ko kwenye furaha uzima tele.