Ataniita
| Ataniita | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Composer | Fr. G. F. Kayeta | 
| Views | 8,166 | 
Ataniita Lyrics
- {Ataniita nami nitamwitikia,
 nitamwokoa, na kumtukuza } *2
- Nitakuwa naye taabuni,
 nitamwokoa na kumtukuza
- Kwa siku nyingi nitamshibisha,
 Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
- Kwa kuwa amekaza kunipenda,
 Nitamwokoa; na kumweka mahali palipo juu.
- Kwa kuwa amenijua jina langu,
 Ataniita nami nitamwitikia.
 
  
         
                            