Yesu Wangu Niokoe
| Yesu Wangu Niokoe | |
|---|---|
| Performed by | St. Maurus Kurasini |
| Album | Hubirini Kwa Kuimba |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | A. K. C. Singombe |
| Views | 10,660 |
Yesu Wangu Niokoe Lyrics
Yesu wangu niokoe,
{ Ulimwegu nilimo ni wa mateso
Nishike mkono wangu Bwana niokoe
Ulikuja duniani kwa wadhambi,
Nitakase kwa damuyo Bwana nitakate
Bwana nakukimbilia } *2- Nionyeshe uso wako uso mkunjufu, nisamehe dhambi,
Nakusihi Mwokozi, Bwana unisikie - Nimefanana na mwana mwana mpotevu, dhiki na karaha
Vimenisonga sana Bwana unisikie - Wewe ndiwe ngome yangu ngao yangu tumaini langu
Ninakutegemea Bwana unisikie - Roho yangu mwili wangu vyote ni vyako ndivyo ulivyoumba
Viimarishe Bwana, Bwana unisikie - Mungu Baba Mungu mwamba Mungu mkombozi
Mungu wa mapaji, Utatu Mtakatifu usifiwe milele