Hapa We Msafiri
Hapa We Msafiri |
---|
Performed by | - |
Category | Mazishi |
Composer | Fr. G. F. Kayeta |
Views | 10,172 |
Hapa We Msafiri Lyrics
- Hapa we msafiri simama na tazama (simama na tazama)
Nimekufa leo, kesho - ni zamu yako
(ona) ona vema nilivyowekwa humu,
Na nilivyoacha mali na jamaa
- Nilitoka uchi tumboni mwa mamangu . . .
Narudia uchi, kati-ka tumbo la nchi
(Sanda) sanda moja hilo ni vazi langu,
Wameninyang'anya hata senti moja.
- Nifunike vema na hilo jembe lako . . .
Nalitangatanga, kati-ka ulimwengu
(Basi) basi leo kiburi kimekwisha,
Kumbe dunia hii ni mti mkavu.
- Nyumba yangu leo ni shimo udongoni . . .
Hakuna mlango, haku-na madirisha
(Kita) kitanda changu na blanketi langu,
Ni udongo mzito wanielemea
- Kifafanuacho wafu mbele ya Mungu . . .
Si cheo kikubwa, si da-raja si sifa
(Mate-) matendo mema saa ya kufa kwangu,
Yatafungua mlango wa uwingu
- Ole wangu mimi nilifanya ujinga . . .
Kwa kuambatana, na wa-tu wa dunia
(Ona) ona wote leo wameniacha,
Hasa watu wale niliowapenda.
- Unapojiona jiwazie mwenyewe . . .
Kufa siku moja, kwa wo-te ni lazima
(Japo) japo sultani japo ni mtumwa,
Mungu atamwita ikiwa saa yake.
- Nimekufa leo nilipona salama . . .
Nalijidhania, mwenye - afya mwilini
(na ma-) na mara moja nikaanguka chini
Labda huamini kwamba nali`mzima.
- Yesu msalabani kateswa vikali mno . . .
Kwa kutukomboa, aka-mwaga damuye
Wahurumie wote wa toharani,
Mwanga wa milele uwaangazie.
- Kwaherini wote kwaherini wapenzi . . .
Ninakwenda kwetu sita-rudi nyuma
(Kwa he-) Kwaheri Baba kwaheri Mama yangu,
Mungu akipenda kwake tukutane.