Mimi Ni Mtumishi

Mimi Ni Mtumishi
Performed byShirikisho la Kwaya Katoliki Dsm (Shikwaka)
AlbumKaribu Tanzania
CategoryBikira Maria
ComposerFr. G. F. Kayeta
Views7,529

Mimi Ni Mtumishi Lyrics

  1. { Mimi ni mtumishi wake Bwana, nitendewe ulivyonena *2
    Nitendewe ulivyonena, mimi ni mtumishi wa Bwana } *3

  2. Salamu uliyejaa neema, Bwana yu pamoja nawe
    Usiogope Maria, Mungu kakupendelea
  3. Tazama utapata mimba utazaa mwana, utamwita jina Yesu,
    Huyu atakuwa mkuu, ataitwa mwana wa aliye juu
  4. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi, cha Baba yeke Daudi
    Ataitawala nyumba ya Yakobo hata milele
    Ufalme wake hautakuwa na mwisho