Tutawapeni Mapesa
Tutawapeni Mapesa | |
---|---|
Alt Title | Haya Enyi Makamanda |
Performed by | St. Charles Lwanga Yombo Dovya Dsm |
Album | Kafufuka Mwokozi |
Category | Pasaka (Easter) |
Composer | A. S. Haule |
Views | 8,097 |
Tutawapeni Mapesa Lyrics
Haya enyi makamanda, leteni mchango wenu *2
Nguvu ya hoja itawa-ale,
Hawa walinzi wameleta habari kuwa kweli amefufuka, amefufuka *2
Sikieni mimi natoa hoja ya nguvu, hoja yangu kweli ya nguvu
Jambo hili likisikika, likisikika katika Uyahudi
Na Samaria itakuwaje aibu hiyo elezeni *2- Hivyo ninyi walinzi, seme-ni
Wanafunzi wake wamemwiba Bwana wao *2
Sisi tulipokuwa tumelala *2 - { (Tutawapeni mapesa) tutawapeni mapesa,
Tutawajaza mapesa, mapesa mtajazwa } *2
Na msiogope kwa ajili ya hilo * 2
{ Wakuu wa nchi wakisikia tutaongea nao
Wakuu wa nchi hao tutasema nao } *2
a. Siku ile ya kufufuka Bwana, maaskari walitetemeka
Wakaenda kwa upesi kumwona jemedari mkuu kumpasha habari - b. Jemedari akafadhaika akawaita watu pamoja kwa shauri;
Wakafanya shauri juu ya jambo hili lipate sura, sura mpya. - c. Dunia yetu siku hizi yafananaje na haya mambo yaliyotokea;
Ukweli unapindishwa ili lile la uongo liwe kweli
Also recorded by St. Cecilia Arusha