Nikitazama Pande Zote
| Nikitazama Pande Zote |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Zaburi |
| Composer | D. Wasonga |
| Views | 3,735 |
Nikitazama Pande Zote Lyrics
Nikitazama pande zote, pande za dunia,
Nikiinua macho yangu niitazame dunia;
Naiona kazi tukufu,kazi ya mikono yako *2
- Wewe Bwana hakika wavipenda vitu vyote,
wavipenda vitu vyote, vitu vyote vilivyomo,
vitu vyote vilivyomo ni kazi yako tukufu
- Wala hukichukii chochote ulichokiumba,
wala hukichukii chochote ulichokiumba,
kwani hivyo vyote ni kazi ya mikono yako.
- Kaskazini na kusini mashariki hata magharibi,
pande zote za dunia zadhihirisha utukufu wako,
zadhihirisha utukufu wako,utukufu wa kazi yako
- Jinsi jina lako lilivyo tukufu ndivyo kazi
ya mikono yako ilivyotukuka duniani,
kazi ya mikono yako imetukuka duniani kote.