KRISTU PASKA YETU
   
    
     
        | KRISTU PASKA YETU | 
|---|
| Performed by | - | 
| Album | Bwana Kafufuka | 
| Category | Pasaka (Easter) | 
| Composer | H. Matete | 
| Views | 8,953 | 
KRISTU PASKA YETU Lyrics
 
             
            
 Kristu Paska yetu amechinjwa sadaka,
 tuile karamuye, tuimbe aleluya *2
 
 Aliyejitoa sadaka ya Paska, wakristu wamtolee sadaka ya sifa
 Mwanakondoo (amewakomboa) mwanakondoo (Bwana Kristu) asiye na dhambi,
 Amewapatanisha watu wenye dhambi na Baba yake
- Mauti na uzima vimeshindana ajabu
 Kuwa mzima aliyekufa atawala mzima
 Utuambie Maria uliona nini, uliona nini njiani mama
 Niliona kaburi la Kristu ni mzima,
 na utukufu wake Bwana Yesu aliyefufuka (kweli)
- Mashahidi ni malaika, leso ya uso na mavazi,
 Kristu tumaini langu kafufuka * 2
 Twajua Kristu amefufuka,
 katika wafu ewe mfalme mshindaji utuhurumie,
 amina, aleluya