Ni Furaha Duniani
Ni Furaha Duniani |
---|
Performed by | - |
Album | Bwana Kafufuka |
Category | Pasaka (Easter) |
Composer | Deo Mhumbira |
Views | 3,573 |
Ni Furaha Duniani Lyrics
- Ni furaha duniani, Mwokozi kafufuka aee kafufuka
Ni furaha duniani, Mwokozi kafufuka aee kafufuka
Asubuhi na mapema (kafufuka)
Siku ya mwanzo ya juma (kafufuka)
Ameyashinda mauti (kafufuka)
- Njooni tumshangilie Bwana amefufuka aee kafufuka
Nyimbo nzuri tumwimbie Bwana amefufuka aee kafufuka
- Maria Magdalena kaenda kaburini aee kaburini
Marashi na manemane kaleta kaburini aee kaburini
- Malaika kawambia hayuko kafufuka aee kafufuka
Kawambia wanafunzi hayuko kafufuka aee kafufuka