Nimemaliza
Nimemaliza |
---|
Alt Title | Nimeumaliza Mwendo |
Performed by | - |
Album | Mlipuko wa Sifa |
Category | Tafakari |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 21,286 |
Nimemaliza Lyrics
{ Nimeumaliza mwendo nimeumaliza,
Nimevipiga vita vilivyo vizuri
Nimeumaliza mwendo nimeumaliza,
Imani nimeilinda nimeilinda } * 2
- Ninakuamuru mbele ya Mungu mbele ya Yesu
Nenda ukauhubiri ule ujumbe
wakati ufaao na wakati usiofaa
Kemea, karipia, onya, himiza
- Wafundishe watu wafundishe kwa uvumilivu
Utakuja wakati, ambapo watu,
hawatasikiliza mafundisho ya ukweli
na kisha kufuata tama zao
- Watakataa kuisikiliza iliyo kweli,
Watajikusanyia walimu tele
Wanaofundisha lipendezalo sikio lao
Lakini, uwe macho, uvumilie
//hitimisho//
Nilipojitetea mara ya kwanza hakuna mtu
Aliyesimama upande wangu, waliniacha
Namuomba Mungu asiwahesabie kosa hilo
Na tena namuomba awasamehe
Lakini Bwana Mungu alisimama pamoja nami
Akanitia nguvu na nikaweza kuutangaza,
Ujumbe usikike kwa watu wa mataifa yote kusudi waokolewe
{ Ooh nimewekewa taji ya uzima
ooh oho ambayo Bwana atanivika
Oho oho na wala siyo mimi peke yangu
ooh ooh ho bali na wote aliowapenda }* 6