Ee Bwana Nifundishe Kupenda
Ee Bwana Nifundishe Kupenda Lyrics
Ee Bwana nifundishe kupenda, ee Bwana nifundishe kutumikia
Ee Bwana nifundishe (kuwajua wenzangu ee) Ee Bwana nifundishe kutumikia
- Nifanye juhudi kuwajua watu, kusudi nizifahamu shida zao
Nisiwape kazi kubwa kutafuta njia ya kunieleza shida zao
Nisiwe mwenye haraka kuwachoka, niliowasaidia mara nyingi
Nijue kusaidia ni safari, iliyo na milima mingi na miiba
- Nijue kuwatetea wadhaifu, wasipoteze thamani nikiona
Maana hawakuchagua hali yao. Wamekuwa hivyo kusudi utukuzwe
Nijibidiishe daima kutafuta, kuwasiliana na jamaa zetu
Kwa kuwa mahusiano ni gharama, hayawezi kuwepo bila jitihada
- Maana nikishajua kupenda, na nikazingatia kutumikia
Kilicho nileta hapa duniani, kitakuwa kimetia niondoke