Kimulimuli
Kimulimuli | |
---|---|
Performed by | St. Joseph the Worker Ngokolo Shinyanga |
Album | Njooni Tumsifu Mungu |
Category | Tafakari |
Composer | F. E. Nyanza |
Views | 3,356 |
Kimulimuli Lyrics
- Kimulimuli chamulika pande zote za dunia
Ngurumo zake zasikika, zasikika kote
ona matetemeko ya ardhi, hata na vita
pia na njaa nayo magonjwa yasipona
Tuyakumbuke yale yaliyotabiriwa na manabii
ya kuwa siku za mwisho yatatokea haya
Tujiweke tayari atakapokuja Bwana wa mavuno
Mbingu na nchi zitapita
Neno la Mungu litadumu
Tujiweke tayari atakapokuja Bwana wa mavuno
Tujiweke tayari
{Tujitakase, tujitakase, tujiweke tayari
Tujitahidi, tubadili mwenendo wa maisha
Kwa kuwa hatujui siku wala saa }* 2 - Tumuombe sana Mungu arudishe huruma yake
Tuweze kushinda haya yote