Sauti Inavuma
   
    
     
         
          
            Sauti Inavuma Lyrics
 
             
            
- Sauti inavuma (kulia), sauti inavuma (kushoto)
 Sauti inavuma pande zote zinatikisika ulo
 Dunia inanesa (kabisa), mbingu zinafurahi (lazima)
 Watumwa wako huru, wanaimba na kumshukuru Mungu
 Hii ni siku yetu, ya kubadilika na kutakata
 Kuvua utu wa kale, na kuvaa, kuvaa utu mpya leo
 Kwani mwalimu wetu, walimning`iniza na kumuua
 Kaachana na kaburi ni mzima kama alivyokuwa mwanzo
 Tunaimba aleluya, eeh eh aleluya,
 Tunaimba aleluya, tunamshukuru aliye juu
 Ngoma tunamchezea, tunamchezea,
 Vigelegele vya nguvu vinaambatana na makofi
 Tunapiga makofi makofi, makofi tu.
- Ya kibinadamu kayaishi kama, kama vile tulivyo sisi (kabisa)
 Na halafu akabadilika akavaa mwili wa utukufu
- Lengo lake atuelimishe hivi, hivi kabisa tulivyo sisi (kabisa)
 Tujitahidi kubadilika na kuvaa hali ya utukufu
- Tukubali maumivu yote tena tujikane bila kusaza (fahali)
 Makusudi tuzisalimishe hizi nafsi zetu kwa Mungu wetu