Basi Mkiwa Mmefufuliwa
   
    
     
         
          
            Basi Mkiwa Mmefufuliwa Lyrics
 
             
            
- { Basi mkiwa mmefufuliwa, pamoja na Yesu Kristu
 Yatafuteni yaliyo juu Kristu aliko
 Ameketi mkono wa kuume,
 mkono wa kuume wa Mungu } * 2
- Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi
 Kwa maana mlikufa na uhai wenu
 Umefichwa pamoja na Kristu katika Mungu
- Kristu atakapofunuliwa, aliye uhai wetu
 Ndipo na ninyi mtafunuliwa
 Pamoja naye pamoja naye katika utukufu
- Lakini sasa Kristu amefufuka, amefufuka katika wafu
 Limbuko lao waliolala, maana mauti ililetwa na mtu
 Kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu