Tazama Mimi Namshukuru

Tazama Mimi Namshukuru
Performed byKwaya ya Malkia wa Mitume Parokia ya Vincent Palloti Arusha
AlbumDira
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerVictor Aloyce Murishiwa
Views4,092

Tazama Mimi Namshukuru Lyrics

 1. {Tazama Mimi ninamshukuru Mungu (wangu) (mimi)
  Najizungusha, mimi kwa nyimbo za shangwe }* 2
  {Twende aiyeye aiyeyeye piga makofi
  (Aiye iye) aiyeye aiyeyeye njooni tucheze wote
  aiyeye aiyeyeye piga makofi
  (Aiye iye) Aiye aiyeyeye tumshukuru Mungu

 2. {Tazama Mungu jinsi alivyoniumba,
  Jinsi hii ni ajabu na yenye kutisha aha }* 2
 3. Nitaimbaje ili wote wasikie,
  Zeze rumba, tarumbeta au madowazi aha
 4. Nitafurahi mimi nitashangilia,
  Kwa furaha nitaimba nyimbo za masifu aha
 5. Nakushukuru Mungu kwa kila sauti,
  Kinywa changu kitatangaza matendo yako aha
 6. Milima yote nanyi mabonde sifuni,
  Kwa kinanda na bahari icheze midundo aha